SERIKALI imeridhishwa na utoaji wa huduma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), hususan katika kurahisisha upatikanaji wa huduma zake.
Akitembelea mabanda ya washiriki katika Kongamano la Manunuzi lililofanyika Mkoani Arusha, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Ridhiwan Kikwete, alionesha kuridhishwa na huduma zinazotolewa kwa wanachama.
“NHIF kwa sasa mnakwenda vizuri hususan katika utoaji wa huduma zenu ambapo kwa sasa mwananchi anaweza kujisajili kwa njia ya mtandao, endeleeni kuwafikia wananchi ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote,”
NHIF imeshiriki kongamano hilo kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake.
BIMA YA AFYA KWA WOTE, JIUNGE SASA
Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu akitoa maelezo ya maboresho ya mifumo yaliyofanywa na NHIF kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na watu wenye ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipotembelea banda la NHIF katika kongamano la manunuzi mkoani Arusha.