NHIF YAUNGURUMA TAMASHA LA TWENDE ZETU KWA YESU

Imewekwa: 22 June, 2025
NHIF YAUNGURUMA TAMASHA LA TWENDE ZETU KWA YESU

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeshiriki Tamasha la Twende Zetu kwa Yesu kwa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.

Tamasha hilo ambalo limefanyika leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, Mfuko ulipata fursa ya kuelezea umuhimu wa wananchi kuwa kwenye mfumo wa bima ya afya.

Akizungumza katika Kongamano hilo, Meneja Masoko wa NHIF Bi. Anjela Mziray alisema kuwa huduma zinazotolewa na Mfuko zimelenga kuwahakikishia wananchi usalama wa afya zao kwa kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote.

“NHIF tupo hapa kuwahamasisha mjiunge na huduma zetu, sisi tumejipanga kuwafikia kila mlipo ili tuwasajili na tuwape huduma bora zaidi,” alisema Bi. Mziray.

Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakitoa Elimu ya Bima ya Afya katika Tamasha la Twende Zetu kwa Yesu linalofanyika katika uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa gharama zilizowekwa kwa ajili ya kujiunga ni nafuu ikilinganishwa na gharama halisi za matibabu zilizopo kwa sasa.

Wananchi walioshiriki kongamano hilo waliitika kwa shangwe ikiwa ni ishara ya kuikubali NHIF na huduma zake.

Katika kuhakikisha wananchi wanajiunga kwa urahisi, Mfuko umewezesha mifumo yake ambapo mwananchi anaweza kujiunga popote alipo kwa njia ya mtandao.

BIMA YA AFYA KWA WOTE, JIUNGE SASA