Uongozi wa NHIF umefanya kikao kazi na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kuboresha huduma kwa wanachama wa NHIF wanaopata matibabu katika hospitali hiyo ya kibingwa.
Pia Katika kikao hicho, wamejadili:
✅ Njia za kuboresha uchakataji wa madai ya matibabu
✅ Kupunguza makosa ya madai yanayopelekea kukataliwa kwa malipo
✅ Changamoto za kiutendaji zilizojitokeza awali na namna ya kuzitatua kwa pamoja
Kikao hiki kimekuwa na manufaa makubwa katika kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati bora ya utoaji huduma bora kwa wanachama wetu.
NHIF itaendelea kushirikiana na taasisi za afya ili kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma bora, kwa wakati, na kwa ufanisi zaidi.
Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa katika picha ya na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya majadiliano ya uboreshaji wa huduma kwa wananchama wake yaliyofanyika katika ukumbi NHIF jijini Dodoma
\#NHIF #Muhimbili #AfyaBoraKwaWote #Tanzania #BimaYaAfya #HudumaBora