Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, ametembelea banda la NHIF na kujionea namna Mfuko ulivyoboresha utoaji wa huduma kupitia mifumo ya kidijiti ambapo alioneshwa namna mtu anavyoweza kujisajili mwenyewe kupitia mtandao wa NHIF Jihudumie (NHIF self service) na kupata kadi mtandao (e-card) ambayo mwanachama anaweza kutumia kupata huduma za matibabu.
Haya yametukia katika ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayoendelea kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Aidha, alijulishwa kwamba Mfuko umefanikiwa kuunganisha mifumo yake na NIDA pamoja na Taasisi nyingine ambapo sasa mwanachama anaweza kutumia namba yake ya kitambulisho cha Taifa kupata matibabu kwenye vituo vya huduma, bila kuwa na ulazima wa kadi halisi ya NHIF.
Pia, kupitia mifumo mwanachama anaweza kuona taarifa zake za uanachama, kuongeza wategemezi na kutoa maoni.
Dkt. James Msafiri akitoa elimu ya usajili kwa njia ya mtandao kwa mwanachama aliyetembelea banda la NHIF katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma