Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo amekutana na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Morogoro na kuiagiza kubuni na kuendeleza mikakati ya kuimarisha huduma na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiunga na kunufaika na Mfuko huo ili kufikia azma ya Serikali ya Afya Bora kwa wote.