Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Bohari ya Dawa ya Uganda (NMS), wamepongeza kazi inayofanywa na NHIF katika utoaji wa huduma baada ya kikao na uongozi wa NHIF na kuona wanachama wanavyopata huduma katika Hospitali ya Muhimbili. Ziara hiyo ina lengo la kupata uzoefu wa uanzishaji na uendeshaji wa Mfuko wa Bima ya Afya.