SERIKALI YAIPONGEZA NHIF UTEKELEZAJI WA SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Imewekwa: 09 July, 2026
SERIKALI YAIPONGEZA NHIF UTEKELEZAJI WA SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

DSM. 08.07.2026
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ametembelea banda ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ( Saba Saba) maonesho yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wadau kwenye banda la NHIF katika maonesho haya Dkt. Magembe alitumia fursa hiyo kuipongeza NHIF kwa jitihada kubwa zilizofanywa na Mfuko kwenye utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Mfuko katika kutimiza azma ya serikali ya kuhakikisha watanzania wote wanakuwa na bima ya afya, natambua kwa sasa NHIF mmefikia watanzania zaidi ya asilimia 10.2 kutoka asilimia 8 za awali, alisema Dkt. Magembe.


Aidha Dkt. Magembe alisema, natambua kwa sasa mnaendelea na zoezi awamu ya kwanza la usajili wa kaya zisizo na uwezo kupitia kifurushi cha faraja kote nchini, niwapongeze tena NHIF na wadau wengine kwa mafanikio yaliyofikiwa katika zoezi hili kote nchini. Natambua awamu ya kwanza ililenga kufikia kaya 276,004 zenye wanufaika zaidi ya 1.4 milioni, kazi kubwa imefanyika kwa kufikia kaya zaidi ya 172,000 na wanufaika zaidi ya 463,000 wamesajiliwa. Jitihada zote hizi ni nia thabiti ya serikali kuhakikisha umma wa watanzania unapata matibabu kwa mfumo wa bima.
Vile vile nitumie fursa hii kuwa kutoa taarifa kwa wananchi wote kuwa usajili kwa watanzania wote kupitia kifurushi cha Faraja utaanza wakati wowote kutoka sasa, natambua shauku kubwa waliyonayo wananchi kusajiliwa kupitia kufurushi hiki, alisema Dkt. Magembe.
Kwa sasa wakati tunasubiri kifurushi cha Faraja, endeleeni kujiunga na vifurushi vilivyopo NHIF kama Tarangire Afya, Ngoringoro Afya, Mikumi Afya,Tanzanite Afya na Tanzanite Afya. Vifurushi hivyo vinatoa huduma za afya kote nchini kwenye vituo zaidi ya 10,000 kote nchini.
Hata hivyi niwasihi NHIF, endeleeni kutoa elimu na kusajili wanachama kote nchini, ili kufikia malengo yaliyowekwa, alisema Dkt. Magembe.

slot gacor