RC - Dodoma na DG - NHIF Wateta Kuhusu Bima ya Afya kwa Wote

Imewekwa: 17 October, 2025
RC -  Dodoma na DG -  NHIF Wateta Kuhusu Bima ya Afya kwa Wote

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rose Senyamule amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene C. Isaka kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwenye utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Mkurugenzi Mkuu  alimjulisha Mkuu wa Mkoa jinsi NHIF ilivyojipanga kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, "Mfuko umeandaa vifurushi mbalimbali vinavyokidhi mahitaji ya makundi mbalimbali pamoja na maboresho mbalimbali ya mifumo ya utoaji huduma" alisema Dkt. Isaka.

Aidha, katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa aliahidi kushirikiana na NHIF hasa kwa ku alika NHIF kwenye mikutano Mkubwa inayoendelea Mkoani wa Dodoma.
 
 Mkurugenzi Mkuu alimshukuru sana  Mkuu wa Mkoa, aliomba Mfuko kushirikishwa kwenye fursa mbalimbali za mkoa zinazokusanya watu wengi ili kutoa elimu na kusajili wanachama wapya.

Dkt. Isaka alipongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla kujenga Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali maeneo mbalimbali, hali inayopelekea wananchi kupata huduma karibu na maeneo yao.  NHIF imesajili zaidi ya vituo vya afya 450 mkoani Dodoma ili kusogeza  huduma kwa wananchi.

" Nawapongeza sana NHIF kwa jitihada zilizofanyika, hivi sasa malalamiko yamepungua. Ofisi yangu iko wazi wakati wowote pale itakapohitajika" alisema Mhe. Senyamule.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa