Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza katika Tuzo za Ubora za Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA Excellence Awards) kwa mwaka 2025.
Mfuko umeibuka mshindi wa KWANZA katika kundi la Taasisi zinazotoa Bima ya Afya. NHIF imeongoza katika uzingatiaji wa sheria na kanuni (Regulatory Compliance), utawala bora, Uimara wa kifedha (Financial Soundness) na utendaji wa shughuli za bima (underwritng Performance) kwa mwaka 2025.
Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Sekta Bima inayoandaliwa na kutolewa Msimamizi wa Sekta ya Bima (Tanzania Insurance Regulatory Authority- TIRA. Hiki ni kielelezo cha juhudi za Mfuko katika kuimarisha mifumo ya usimamizi na uendeshaji, kuzingatia matakwa ya kisheria na kuhakikisha kuwa shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uwazi na ufanisi.

Ushindi huo unaonesha jitihada za Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na watumishi wa NHIF katika kufuata Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na Utawala bora. Hivyo Mfuko umeomarika ki-mapato na kuwafikia wananchi kwa wingi. Mfuko umechangia kuimarisha sekta ya bima nchini, kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na mamlaka za usimamizi Bima .
Eneo jingine lilikuwa ni utawala bora ambapo Mfuko umeonesha umuhimu wa mifumo madhubuti ya usimamizi, uwajibikaji na utoaji wa maamuzi yanayolenga kulinda maslahi ya Mfuko na wanachama, wadau na nchi kwa ujumla
Kwa upande wa uimara wa kifedha, tuzo hiyo imetambua usimamizi makini wa rasilimali za Mfuko na kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu yake na kuendeleza huduma za bima ya afya kwa wote.
Tuzo hiyo pia imeangalia utendaji katika shughuli za bima (underwriting performance) ambapo tathmini na usimamizi wa vihatarishi vya bima vinafanyika kwa umakini, kwa lengo la kuimarisha uendelevu wa kifedha na uwezo wa Mfuko kutimiza wajibu wake.
Tuzo ya TIRA Excellence Awards 2025 ni alama ya kutambua ubora wa NHIF katika kundi la Bima ya Afya na hamasa ya kuendeleza utendaji bora kwa manufaa ya wanachama na sekta ya afya nchini hasa kwenye utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.