Dodoma, 05/10/2025 Dodoma
Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameungana na maelfu ya washiriki kwenye mbio za Capital City Marathon zilizofanyika jijini Dodoma.
Ushiriki wa mbio hizo ni juhudi ya Menejimenti ya Mfuko katika kuhamasisha afya bora za watumishi kupitia mazoezi na kujenga mshikamano na umoja kwa watumishi toka ofisi mbalimbali nchini.
Ushiriki huu pia ni sehemu ya mkakati wa Mfuko kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa sugu yasiyoambukiza (NCDs) kama vile kisukari na shinikizo la damu.
Kwa niaba ta watumishi walioshiriki mbio hizo toka ofisi mbalimbali za Mfuko, Meneja Udhibiti Udanganyifu Dkt. Rose Ntundu ametoa shukrani kwa Menejimenti kwa fursa za kushiriki marathon na michezo mbalimbali, aidha amewapongeza watumishi wote walioshiriki mbio hizo.
Bima ya Afya kwa Wote. Jiunge Sasa