Dar es Salaam
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeshiriki katika Kongamano la Afya Tanzania (Tanzania Health Summit -THS) linalofanyikia katika ukumbi wa JNICC ambapo Meneja wa Mkoa Kinondoni Dkt. Raphael Mallaba alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene C. Isaka katika mjadala wa mazungumzo (panel discusion) uliohusu kuelekea utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote UHI na somo tulilojifunza toka utekelezaji wa iCHF.
Mjadala huo umefanyika baada ya mawasilisho mawili moja ikiwa ni utafiti uliofanywa na NIMR na mwingine ni experience toka nchi mbalimbali zinazotekeleza Bima ya Afya kwa Wote (UHI) duniani.
NHIF imeonesha maandalizi, mikakati na utayari wa utekelezaji wa bima ya afya kwa wote kwa kuonesha uzoefu wa uendeshaji wa Bima ya Afya kwa zaidi ya miaka 25 sasa.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Mallaba alifafanua mikakati ya usajili wanachama ikiwemo ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ikiwemo kuanza kutumia mawakala wa bima, makampuni ya mitandao ya simu pamoja na kuingia mikataba na mabenki . Pia Mfuko utatumia Maafisa Ustawi wa Jamii (CHW) ambao wako nchi nzima, kutumia mifumo katika usajili(NHIF self-service) pamoja na matumizi ya vitambulisho vya Taifa katika utambuzi wa huduma vituoni.
Aidha mikakati ya kuhakikisha uendelevu wa usajili wa wanachama Mfuko umekuja na mikakati minne ikiwemo;
1. Wanachama kutumia jumbe za meseji kukumbushwa kuhuisha kadi zao zikiambatana na namba za malipo.
2. Punguzo la asilimia 10 (10% discount) kwa wanachama wanaohuisha kadi zao ndani ya wakati ikiwa ni incentive kwao.
3. Mfuko kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa bima ya afya,
4. Mfuko kufuatilia na kusimamia ubora wa upatikanaji wa huduma za afya vituoni.
Aidha, kuhusu suala la utambuzi wa wananchi wanaotoka katika kaya maskini alisema utambuzi wa kaya hizo unafanywa na Wizara ya Afya, TASAF na OR-TAMISEMI ambapo Mfuko utapatiwa majina ya kaya hizo pamoja na michango yao ili kuwaandalia kadi au vitambulisho vya matibabu ambapo wanufaika watahudumiwa katika vituo zaidi ya 10,800 vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima ikiwemo vituo vinavyomilikiwa na serikali, makampuni binafsi na mashirika ya dini.
Kwa upande wake Meneja wa Hadhari na Utafiti wa NHIF Bw. Abubakar Ndwatta alisema katika kuhakikisha kunakuwa na uendelevu (sustainability) ya Mfuko, kwa sasa Mfuko unakamilisha tathmini ya uhai na uendelevu (acturial valuation) ambapo miongoni mwa mapendekezo ni kuwepo kwa udhibiti kwa baadhi ya huduma kama kusafisha damu (dialysis) na matibabu ya saratani (cancer).
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa