MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI (NHIF) MH. ANNE MAKINDA AZINDUA VIFURUSHI VIPYA VYA BIMA YA AFYA “JIPIMIE

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI (NHIF) MH. ANNE MAKINDA AZINDUA VIFURUSHI VIPYA VYA BIMA YA AFYA “JIPIMIE Nov 29, 2019

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya afya vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Makinda akikata utepe wakati wa uzinduzi wa vifurushi vipya vya bima ya afya vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Bernard Konga na kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Tryphone Rutazamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Mh. Peter Serukamba.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Mh. Peter Serukamba akizungumza katika uzinduzi huo.Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Bernard Konga akicheza pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza katika uzinduzi huo.