Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene C. Isaka amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Delilah Kimambo. Mazungumzo hayo yalilenga kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma kwa Wanachama wa NHIF wanaofika kupata huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
NHIF na MNH wameunda timu ya wataalam wabobezi katika Masuala ya Tiba, Uhasibu, Mifumo ya TEHAMA na wataalam wa sheria. Timu hii imepewa Hadidu za rejea kutakiwa kutoa mapendekezo ya maboresho ili kuondoa usumbufu kwa wanachama na wategemezi wao. Ushirikiano huu ni Muhimu katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa wote.
Pamoja na maongezi ya uboreshaji huduma na kuimarisha mahusiano, Dkt. Kimambo alitumia fursa hiyo kujitambulisha, baada kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH hivi karibuni.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Muhimbili, kilihudhuriwa na wataalam wabobezi wa Taasisi zote mbili
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa