Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeendelea kuimarisha mifumo yake ya TEHAMA ambayo inawawezesha watoa huduma kutambua wanachama wa Mfuko wakati wa kupata huduma.

Kutokana na hili Mfuko unapenda kuwakumbusha Waajiri waliosajiliwa na Mfuko kuwasilisha michango ya bima ya afya ya watumishi wao kwa wakati ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa kupata huduma za matibabu.

Mfuko unaendelea kuthamini ushirikiano na Waajiri ili kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma zinazostahili bila usumbufu.

Kwa maelezo zaidi tafadhali piga simu Kituo cha Huduma kwa Wateja (bila malipo) 0800-110063 au tembelea Ofisi ya NHIF iliyo karibu nawe au tuandikie kupitia barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..Atakayesikia tangazo hili tafadhali amtaarifu na mwingine.

Imetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya