MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WANANCHI KWA UJUMLA KUHUSU KUHAMA KWA OFISI ZAKE ZIFUATAZO:-

  1. OFISI ZA NHIF TEMEKE ZILIZOKUWA KATIKA JENGO LA “PETRO MEMBI BUILDING” MKABALA NA HOSPITALI YA WILAYA YA TEMEKE, SASA ZIMEHAMISHIWA KATIKA JENGO LA MEK ONE PLAZA LILILOKO MAKUTANO YA TAZARA KARIBU NA HOSPITALI YA DAR GROUP.
  2. OFISI NHIF ZA ARUSHA ZILIZOKUWA KATIKA JENGO LA MIKUTANO LA KIMATAIFA LA AICC, SASA ZIMEHAMISHIWA KATIKA JENGO LA NSSF KALOLENI.

HUDUMA ZOTE ZA NHIF ZITAENDELEA KUTOLEWA KATIKA OFISI HIZI MPYA.

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UNAOSABABISHWA NA MABADILIKO HAYA.

KAIMU MKURUGENZI MKUU,

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA.