Maktaba ya Picha • 7

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, katika bonanza iliyoandaliwa na Tanzania Insurance Brokers Association (TIBA) siku ya Jumamosi ya tarehe 16/3/2019, umeibuka mshindi na kupokea tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza, katika mashindano ya mpira wa pete na uvutaji wa kamba na pia kushika nafasi ya pili katika...

  Imewekwa : March, 21, 2019

 • 4

  Wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya DSM leo wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea watoto wa Kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Kurasini na wametoa TOTO Afya Kadi na vitu mbalimbali kusaidia mahitaji yao.

  Imewekwa : March, 09, 2019

 • 2

  Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kutoka idara ya Masoko na Huduma kwa wateja wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuboresha huduma za Mfuko na kuwafikia wananchi wote nchini. Mafunzo haya yanaendeshwa na wakufunzi kutoka chuo kikuu Mzumbe.

  Imewekwa : February, 19, 2019

 • 4

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mama Anne Makinda amefunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi mjini Dodoma na kusisitiza watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma lakini pia kuwafikia wananchi wengi zaidi.

  Imewekwa : February, 18, 2019

 • 4

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (katikati) amefungua Baraza la Wafanyakazi la NHIF leo. Baraza hilo litajadili mambo mbalimbali ya uimarishaji wa Mfuko ikiwemo kuweka mikakati madhubuti ya kuwafikia wananchi wa makundi yote.

  Imewekwa : February, 14, 2019